Leo Afrika Ni Ya Moto Kufuzu Kombe la Dunia 2026

Soka la Afrika linaendelea kushika kasi huku hatua ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 ikifikia Raundi ya 8. Timu kadhaa kubwa zipo uwanjani leo, zikisaka pointi muhimu zinazoweza kufungua milango ya kwenda Marekani, Mexico na Kanada mwakani. Baadhi ya michezo mikubw inayosubiri kutazamwa na wengi ni pamoja na;

Leo Afrika Ni Ya Moto Kufuzu Kombe la Dunia 2026

Zambia dhidi ya Morocco.

Pambano la kufungua dimba ni la aina yake. Zambia wanakutana na timu bora barani Afrika, Morocco, waliowahi kucheza nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022. Chipolopolo wanahitaji kushinda ili kusalia kwenye mbio, lakini Morocco wana kikosi kilichojaa nyota wa Ulaya huku wakiwa wamefuzu tayari.

Mozambique dhidi ya Botswana.

Mozambique wakiwa Maputo wanataka kuendeleza mwendo mzuri, lakini Botswana wameonyesha uimara katika mechi za hivi karibuni. Ni mchezo wa pointi tatu unaoweza kubadilisha nafasi za kati ya kundi. Huku mchezaji wa kuangaliwa kwa upande wa Mozambique akiwa ni Geny Catamo anayecheza Sporting Lisbon anayesifika kwa kuwa na kasi na uwezo wa kufunga.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Guinea dhidi ya Algeria(Casablanca)

Guinea pamoja na kuwa mwenyeji wa mchezo huu kiratiba lakini wanacheza ugenini kutokana na changamoto za viwanja, huku wakikabiliana na Algeria waliokomaa. Algeria wakishinda, wanaweza kufuzu rasmi. Huu mchezo unawakutanisha nyota wakubwa barani Afrika, Riyad Mahrez anayecheza Al Ahli na Serhou Guirassy anayekipiga Stuttgart.

Leo Afrika Ni Ya Moto Kufuzu Kombe la Dunia 2026

Ghana dhidi ya Mali 

Hii ndiyo gemu inayovuta macho ya mashabiki barani. Ghana na Mali wamekuwa wapinzani wa muda mrefu, na kila upande unakuja na nyota wanaong’aa Ulaya. Pointi tatu hapa zinaweza kuamua mustakabali wa kundi lote. Baadhi ya nyota tutakaowashuhudia kwenye mchezo huu ni pamoja na Mohammed Kudus (West Ham) na Thomas Partey (Arsenal) kwa upande wa Ghana, huku upande wa Mali wakiwa ni  Amadou Haidara (RB Leipzig), na Sekou Koita (Red Bull Salzburg).

Leo ni siku ya maamuzi. Tunisia na Algeria wanaweza kutinga Kombe la Dunia rasmi, wakati pambano la Ghana dhidi ya Mali linaweza kuwa kipimo cha nani atakayeongoza kundi lao. Afrika nzima inashuhudia, je, nani ataibuka kidedea?

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.