Liverpool Bado Wanaivizia Top Four

Klabu ya Liverpool bado hawajaikatia tamaa nafasi kua kwenye timu nne za juu ambazo zitashiriki ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao baada ya kufanikiwa kushinda mchezo wake dhidi ya Tottenham katika dimba la Anfield leo.

Liverpool wamefanikiwa kupanda mpaka nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuichapa klabu ya Tottenham Hotspurs kwa mabao manne kwa tatu na kufufua rasmi matumaini ya kumaliza kwenye nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.LiverpoolVijogoo wa Anfield walifanikiwa kupata mabao matatu ndani ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Curtis Jones, Luiz Diaz, na Mohamed Salah huku Tottenham nao wakipata bao moja kupitia kwa Harry Kane na mchezo kwenda mapumziko Spurs wakiwa nyuma kwa mabao matatu kwa moja.LiverpoolKipindi cha pili kilianza kwa Tottenham wakionekana kuhitaji kusawazisha mabao ambayo wametanguliwa kutokana na kasi ambayo walianza nayo na ndivyo ilivyokua kwani dakika ya 77 Heung Ming Son aliipatia bao la pili Spurs kabla ya Richarlison kusawazisha dakika za nyongeza na kufanya ubao kusomeka 3-3, Lakini Diogo Jota dakika ya 94 aliipatia Liverpool bao la nne na kuhakikisha alama tatu zinabaki Anfield.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.