Ilikuwa ni uamuzi uliokuja kuwaumiza Liverpool na ambao unaweza kuwagharimu tena siku zijazo.

Huku Mohamed Salah akiwa hafungi mabao mengi au kutengeneza nafasi nyingi kama alivyofanya msimu uliopita, safu ya ulinzi ilihitaji kuwa imara zaidi. Badala yake, imekuwa ikibadilika-badilika kama ilivyo kwa safu ya ushambuliaji.
Kwa kuwa nafasi zote mbili za mabeki wa pembeni zimekuwa na matatizo, Virgil van Dijk amelazimika kumbeba Ibrahima Konaté ambaye amekuwa akifanya makosa mara kwa mara katika sehemu kubwa ya msimu, huku kukiwa hakuna mbadala wa uhakika kutokana na majeraha.
Dirisha la usajili liligeuka kuwa kama hadithi ya “sliding doors” kwa Liverpool, ambapo dili la Marc Guehi lililokuwa tayari kukamilika lilivunjika baada ya Crystal Palace kulisitisha kufuatia Jarell Quansah kuruhusiwa kujiunga na Bayer 04 Leverkusen. Kama mojawapo ya dili hizi ingekwenda sawa, Liverpool wasingerejea kwenye hali ya kuanza upya majira haya ya joto.
Kwa mujibu wa Bild kupitia Bulinews.com, Quansah anatarajiwa kurejea Anfield. Si msimu huu wa joto ambapo kipengele chake cha kuachiliwa ni £80m, bali mwaka ujao ambapo kitakuwa “tu” £60m na wakati mkataba wa Virgil van Dijk utakapomalizika.

Richard Hughes alifanya mambo mengi sahihi, lakini Quansah angeweza kutolewa kwa mkopo badala ya klabu kutumia pauni milioni 30 kumsajili mchezaji ambaye kwa muda mrefu ameonyesha uwezo wa kuwa chaguo la kudumu Anfield, iwe kama beki wa kati au beki wa kulia.
Mchezaji huyo mwenye miaka 22 ameendelea kuimarika katika Bundesliga, lakini amesisitiza kuwa muda wake Liverpool ulikuwa muhimu kwa maendeleo yake, akizungumza kupitia The Guardian:
“Daima nimejifunza kutoka kwa baadhi ya wachezaji bora niliokuwa nao Liverpool na hilo limekuwa jambo zuri sana kwa maendeleo ya kazi yangu. Lakini kama beki wa kati kijana, unahitaji kucheza mechi nyingi na ninahitaji mamia ya mechi kufika pale ninapotaka kuwa.” Alisema

“Nilitaka muda wa kucheza, na unapokuwa kwenye timu kama Liverpool, hilo haliahidiwi kwa sababu kuna wachezaji wa kiwango cha dunia kila sehemu ya uwanja. Nilihitaji sehemu ambayo watanipa nafasi hata nikikosea mara chache, lakini wataona uwezo wangu wa kuendelea kusonga mbele.”
Huenda bado hajafikia kiwango cha dunia, lakini kama ataendelea kwa kasi hii ya maendeleo, hatakuwa mbali kufika huko.