Klabu ya Liverpool imepoteza mchezo wake wa pili kwenye ligi mfululizo hapo jana baada ya kutandikwa na Leeds United kwa mabao 2-1 akiwa nyumbani kwake kwenye mchezo uliochezwa majira ya saa 3:45 usiku.

 

Liverpool Yapoteza Mchezo Wake wa Pili Mfululizo Kwenye Ligi.

Leeds United,walikuwa wa kwanza kupata bao ambapo katika dakika ya nne tuu walikuwa tayari wanaongoza na baadae kwenye dakika ya 14 Liverpool wakasawazisha kupitia kwa mchezaji wao Mohamed Salah.

Licha ya vijana wa Klopp kupiga mashuti 10 yaliyolenga lango na kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa lakini walishindwa hata kutoa sare na baadae kufanya makosa yaliyosababisha wapinzani wao wapate bao la ushindi dakika za jioni za 89 kupitia kwa Summerville.

Vijana wa Jesse Marsch baada ya kupata ushindi huo wamepanda hasi nafasi ya 15 huku wakiwa na pointi 12 kwenye msimamo wakati Majogoo wa Anfield wao wakiwa nafasi ya 9 baada ya kupoteza mechi ya jana.

Liverpool Yapoteza Mchezo Wake wa Pili Mfululizo Kwenye Ligi.

Klopp msimu huu ana hali mbaya sana kwani hana mwendelezo mzuri wa matokeo baada ya kuwa na sare nyingi na kupoteza michezo mingi na matumaini ya kupigania ubingwa wa Ligi hiyo kuonekana kutokuwepo kabisa.

Mpaka sasa Leeds amezifunga timu kubwa mbili ambazo ni Chelsea pamoja na Liverpool, na mechi inayofuata watakipiga dhidi ya AFC Bournemouth wakati kwa upande wa Majogoo wao wataumana dhidi ya Napoli kwenye Ligi ya Mabingwa na baadae kuwavaa Spurs.

Liverpool Yapoteza Mchezo Wake wa Pili Mfululizo Kwenye Ligi.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa