Klabu ya Atletico Madrid wameendelea kuchechemea kama ambavyo wamekua katika siku za hivi karibuni. Hiyo imekuja baada ya kukubali kipigo cha mabao matatu kwa mawili na klabu ya Cadiz.

Atletico Madrid wamekua kwenye wakati mgumu siku za hivi karibuni kutokana na matokeo ambayo wamekua wakiyavuna katika michezo yao, jambo ambalo limekua likiwatia mashaka mashabiki wa klabu hiyo wakiamini kama timu yao itaendelea hivi basi wana uwezekano wa kukosa nafasi nne za juu.atletico madridKatika mchezo huo ambao ulipigwa mapema mchana na kushuhudia Athletico wakidondosha alama zote tatu mbele ya Cadiz, Ulikua mchezo ambao klabu iliutawala lakini vijana wa Cadiz walionekana kucheza kwa nidhamu na kushambulia kwa kushtukiza.

Vijana wa Simeone wamekua kwenye wakati mgumu tena leo ni baada ya kusuluhu katikati ya wiki kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya, Na kutupwa nje ya michuano hiyo baada ya kushindwa kufuzu hatua ya 16 bora.real madridKutokana na kitendo hicho na matokeo ya leo inaonesha Atletico Madrid bado wanaishi kwenye jinamizi la matokeo mabaya, jambo ambalo likiendelea hiuvi litawasumbua na kukosa hata nafasi ya kushiriki michuano ya ulaya msimu unaofuata.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa