Maguire Rasmi Avuliwa Unahodha United

Beki wa kimataifa wa Uingereza Harry Maguire ameeleza kupitia mitandao ya kijamii kua kwasasa sio nahodha tena wa klabu ya Manchester United baada ya mazungumzo ya kina na kocha wa klabu hiyo.

Harry Maguire kupitia mitandao yake ya kijamii aliandika “Baada ya mazungumzo ya kina na meneja leo ameniambia amebadilisha nahodha kutokana na sababu zake alizonieleza, Japo nimekatishwa tamaa lakini nitaendlea kujitolea kila nitakapovaa jezi hii”maguireBeki huyo amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa kumpa ushirikiano kwa kipindi chote cha miaka na nusu alichovaa kitambaa cha unahodha ndani ya timu hiyo, Huku akisema ni miongoni mwa mambo ambayo anajivunia katika maisha yake ya soka kuiongoza klabu kubwa kama Man United.

Beki Harry Maguire pamoja na kutoa shukrani kwa mashabiki lakini hakumsahau aliyekua kocha wa klabu Ole Gunnar Solskjaer ambaye ndio alimpa jukumu la kua nahodha wa timu hiyo kwa mara ya kwanza na kusema atamkumbuka miaka yote kwa kumpa nafasi hiyo.maguireBaada ya Maguire Kuvuliwa kitambaa cha unahodha ndani ya timu hiyo hii inaendelea kuonesha kila dalili kua huenda zama za beki huyo ndani ya klabu hiyo zimefika mwisho, Huku klabu kadhaa zikielezwa kuulizia huduma ya beki huyo wakiwemo klabu ya West Ham chini ya kocha David Moyes.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.