Mapinduzi Cup : Simba SC Uso kwa Uso na Azam FC Leo.

Fainali ya Kombe la Mapinduzi inategemewa kuamua bingwa leo katika dimba la Amani, Zanzibar majira ya saa mbili na robo usiku wakati Azam FC watakapovaana na Simba SC.

 

Katika miaka saba iliyopita Simba SC imefanikiwa kutinga fainali mara tano na kushishinda ubingwa mara moja pekee suala ambalo Pablo amesema kesho ni mwisho.

Azam FC ambao ni mabingwa wa historia wa kombe la mapinduzi wamefanikiwa kucheza fainali hizo mara tano na kushinda katika fainali zote huku akiwa na histori aya kumfunga Simba SC katika fainali mbili walizokutana.

Kocha Mkuu wa Simba SC, Pablo amefunguka kuwa kuingia fainali ni jambo zuri lakini kutwaa kombe ni vizuri zaidi hivyo watahakikisha wanapambana kushinda.

“Tangu mara ya kwanza nilivyokuja hapa nilisema malengo yetu ni kutwaa ubingwa, kesho ni fainali na tuko tayari kupambana kuhakikisha tunafikia dhamira hii.

 

“Wachezaji wote wako kwenye hali nzuri, tunategemea mchezo mzuri kama ulivyokuwa katika mechi dhidi ya Namungo. Tunataka kuibadili historia na kushinda taji,” amesema Pablo.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe