Tetesi za Soka Barani Ulaya

 

Tetesi zinasema, Paris St-Germain wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, huku Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 28 pia akitaka kuhamia klabu hiyo ya Ligue 1.

Tetesi zinasema, Manchester United wanamtaka beki wa kulia wa Brighton, Tariq Lamptey. Brighton wanataka pauni milioni 40 kumuuza mchezaji huyo.

Arsenal wamefanya mawasiliano na Juventus kuhusu mkataba wa mkopo wa kiungo wa kati wa Brazil Arthur Melo, 25. Pia wanamlenga kiungo wa kati wa Leicester na Ubelgiji Youri Tielemans, 24.

The Gunners pia bado wanavutiwa na mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic, 21, lakini watakuwa na shida kufadhili uhamisho wa Mserbia huyo kufikia mwisho wa mwezi.

Tetesi zinasema, Meneja wa PSG Mauricio Pochettino bado anawasiliana na Man Utd kuhusu uhamisho wa majira ya joto. Meneja wa sasa wa muda Ralf Rangnick anamtaka bosi wa Ajax Erik ten Hag.

 

Rudiger

Beki wa Chelsea, Antonio Rudiger sasa anapanga kusalia Stamford Bridge. Mjerumani huyo, 28, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao alikuwa akihusishwa na kutaka kuondoka.

Tetesi zinasema, Aston Villa wanawinda saini ya kiungo wa kati wa Brighton Yves Bissouma, 25.

Tetesi zinasema, Leicester City na Filip Benkovic wamekubali kufuta kandarasi ya beki huyo wa Croatia mwenye umri wa miaka 24.

Ousmane Dembele anatazamiwa kuondoka Barcelona mwishoni mwa msimu huu na Manchester United wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24.

Tetesi zinasema, Tottenham wamekataa ombi la winga wa Uholanzi Steven Bergwijn, 24, kutoka Ajax.

Tetesi zinasema, Newcastle wanatayarisha ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa RB Leipzig na Mali Amadou Haidara, 23.

 

Tottenham wanataka kusajili wachezaji watatu muhimu katika dirisha la uhamisho. Spurs wako kwenye mazungumzo na Wolves kuhusu kiungo wa kati wa Uhispania Adama Traore, 25, na wanatafuta beki wa kulia na mshambuliaji.

Newcastle wametuma ofa mpya ya pauni milioni 28 kwa mlinzi wa Sevilla na Brazil Diego Carlos. Hapo awali The Magpies walikuwa na ofa ya pauni milioni 25 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 iliyokataliwa.

Tetesi zinasema, Juventus wana nia ya kutaka kumnunua kwa mkopo mshambuliaji wa Barcelona na Uholanzi Memphis Depay, 27.

Manchester United itaweka kipaumbele kandarasi mpya kwa mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 unakamilika Juni 2023.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.