Ferran Torres Kuanza Kwenye El Classico

Mchezaji mpya wa klabu ya Barcelona Ferran Torres ametajwa kwenye kikosi ambacho kitachuana na Real Madrid usiku wa leo kwenye mchezo wa nusu fainali ya Supercopa de Espana nchini Saudi Arabia.

Mshindi wa kati ya Barcelona na Real Madrid atakutana na mshindi kati ya Athletic Club au Atletico Madrid kwenye mchezo wa fainali ambao unategemea matokeo ya michezo yote mawili.

Ferran Torres
Ferran Torres

Carlo Ancelotti amepanga kutumia mfumo wa 4-3-3 huku kikosi kitachoanza kitakuwa na Thibaut Courtois golini huku kwenye safu ya ulinzi Dani Carvajal, Eder Militao, Nacho na Ferland Mendy, kiungo kukiwa na Casemiro, Toni Kroos na Luka Modric, pia nafasi ya ushambuliaji ikiongozwa na kapteni Karim Benzema, Marco Asensio na Vinicius Junior.

Huku kikosi cha Xavi akitumia mfumo sawa na mpinzani wake 4-3-3, kikoso chake kikiwa na Marc-Andre ter Stegen golini nafasi ya ulinzi Dani Alves, Gerard Pique, Ronald Araujo na Jordi Alba, muhimili wa kati ukiongozwa na Sergio Busquets, Frenkie de Jong, Gavi huku nafasi ya ushambuliaji Luuk de Jong, Ousmane Dembele na Ferran Torres.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe