Sky Sport Italia na Gazzetta dello Sport wanaripoti kuwa AC Milan wana nia ya kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Leon Goretzka, kwa usajili wa bure mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ni miongoni mwa malengo ya Milan kwa dirisha la usajili la majira ya kiangazi ya mwaka 2026.
Mkataba wa kiungo huyo mwenye uzoefu mkubwa na Bayern Munich unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu, na kwa mujibu wa Sky Sport Italia na Gazzetta dello Sport, Rossoneri tayari wameanza kuchunguza uwezekano wa dili hilo kwa kuwasiliana na wakala wa mchezaji huyo.
Kwa mujibu wa Gazzetta, Goretzka ataondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu kwa uhakika, kwani pande hizo mbili hazijawahi hata kukaribia kufikia makubaliano kuhusu kuongeza mkataba wake.


