Mchezaji mahiri mzawa wa Australia, Aaron Mooy, 29, ameelekea nchini China kuchezea Shanghai SIPG baada ya kuagana rasmi na kikosi cha Brighton nchini Uingereza.

 

Mooy Ajiunga na Shanghai SIPG akitokea Brighton.
 

Mooy alisajiliwa na Brighton almaarufu ‘Seagulls’ kwa mkopo kutoka Huddersfield Town mnamo Agosti 2019. Uhamisho huo ulirasimishwa kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.

Akivalia jezi za Brighton, Kiungo huyo aliwajibishwa na kikosi hicho cha Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mara 32 msimu huu wa 2019-20 na akafunga mabao mawili.

 

Mooy Ajiunga na Shanghai SIPG akitokea Brighton.

“Mooy amekuwa mchezaji bora katika kipindi hiki chote akiwa nasi. Uhamisho wake hadi China utamkuza zaidi kitaaluma,” akasema kocha wa Brighton, Graham Potter.

Shanghai SIPG kwa sasa wanashikilia nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa jedwali la Ligi Kuu ya China (Chinese Super League).


Beti Mbio za Mbwa Mubashara

Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.

Cheza Hapa

53 MAONI

  1. Klabu za China zimekuwa zikilipa mishahara mikubwa wachezaji kutoka Ulaya lkn bado haijaweza kuvutia majina makubwa ya wachezaji na haijawa na mvuto #meridianbettz

  2. Bonge la maisha kwa wachezaji ambao wanasajiliwa China huwa wanalipya pesa nyingi sana kiasi kwamba wanapenda hadi kuwa RAIA wa china

  3. Mooy amekuwa mchezaji bora katika kipindi hiki chote akiwa nasi. Uhamisho wake hadi China utamkuza zaidi kitaaluma.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa