Pablo : Tumekuja Kubeba Ubingwa.

 

Kocha mkuu wa Simba SC, Pablo Franco amesema kuwa hawajaenda kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kama washiriki wa michuano, malengo yao ni kuhakikisha wanachukua ubingwa wa kombe hilo kutokana na ukubwa wa timu yao.

 

Pablo ametoa kauli hiyo kabla ya leo Jumatano, Simba kucheza mchezo wake wa kwanza katika michuano hiyo dhidi ya Selem View saa 10:15 jioni kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Pablo alisema: “Malengo makubwa ni kuona katika michuano hii tunaweza kuchukua ubingwa hilo ndiyo jambo kubwa ambalo limetuleta huku kwa sababu hatukuja kama washiriki wa haya mashindano bali tumekuja kama moja kati ya timu washindani ambao tunahitaji kuona tunaondoka na ubingwa.

 

“Nimeambiwa msimu uliopita hatukuweza kufikia malengo kwa sababu tulifungwa na wapinzani wetu Yanga kwenye mchezo wa fainali lakini safari hii naamini tumekuja na timu ambayo inaweza kupata matokeo katika mchezo wowote hadi kufikia malengo yetu na ndiyo ambalo tunaliangalia kupata ushindi kwenye kila mechi ambayo itakuwa mbele yetu.” aliongeza Pablo.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe