Pavlovic Awasili Milan Kukamilisha Uhamisho Wake

Beki wa RB Salzburg Strahinja Pavlovic alitua Milan jana jioni na yuko tayari kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu hiyo.

Pavlovic Awasili Milan Kukamilisha Uhamisho Wake

Beki huyo wa kati wa Serbia mwenye umri wa miaka 23 aliibuka kuwa mmoja wa walengwa wa Rossoneri ili kuimarisha safu ya ulinzi ya Paulo Fonseca msimu huu wa joto kufuatia kipindi cha miaka miwili nchini Austria, ambacho kiliwashawishi Zlatan Ibrahimovic, Geoffrey Moncada na Giorgio Furlani.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Pavlovic Awasili Milan Kukamilisha Uhamisho Wake

Milan wamekubali kumsajili Pavlovic kutoka RB Salzburg kwa dili la takriban euro milioni 18 pamoja na nyongeza za €2m, tayari kushirikiana na Fikayo Tomori.

Wakati huohuo, Newcastle United wanahusishwa pakubwa na kutaka kumnunua Malick Thiaw, na hivyo kutoa nafasi kwenye safu ya ulinzi.

Corriere dello Sport leo inaeleza jinsi Pavlovic aliwasili katika mji mkuu wa Lombardy jana jioni kufanya uchunguzi wake wa afya na sasa yuko tayari kukamilisha uhamisho wake kwenda Milan, huku maelezo ya mwisho sasa yakitatuliwa.

Pavlovic Awasili Milan Kukamilisha Uhamisho Wake

Beki huyo alikataa kuhamia Atletico Madrid ili kusukuma uhamisho wa kwenda Rossoneri. Katika miaka yake miwili na RB Salzburg, mchezaji huyo alifunga mabao sita na kutoa asisti sita katika mechi 71.

 

Acha ujumbe