Ranga Chivaviro Kuhusu Yanga Afunguka.

Ranga Chivaviro mchezaji wa Kaizer Chief ambaye aliwahi kuwindwa na Yanga akachomoa dakika za mwisho, alisema Yanga iliwaweka kwenye wakati mgumu ambapo nidhamu yao wakati hawana mpira ni ilikuwa kitu kigumu kwao kuweza kuhimili. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Ranga Chivaviro mwenye asili ya Zimbabwe, alisema walikutana na kipimo kigumu katika mchezo wa kwanza wa kirafiki tangu waanze maandalizi.

“Ilikuwa ngumu kwetu, ni kama hawakutupa nafasi ya kujipanga wakati tukiwa tuna mpira, walikuwa wanalazimisha haraka tuupoteze uwe chini yao nadhani ndio silaha waliyoitumia kutengeneza ushindi kama ule,” alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Marumo Gallants.

“Unajua huu ulikuwa mchezo wetu wa kwanza wa kirafiki wenzetu walionekana kuwa wepesi kuliko sisi ilitufanya kuonekana hatukuwa tayari kukutana na watu kama wao, nadhani tutabadilika kwa kuwa tupo chini ya makocha wapya ambao wanaaanza kutupa falsafa mpya.” Alisema Chivaviro.

Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 4-0, ambapo walifanikiwa kutwaa taji la Toyota Cup, ikiwa ni kombe lao la kwanza wa msimu wa 2024/25.

Mabao ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji wao mpya, Prince Dube, na Kiungo Stephen Aziz Ki, alifunga mabao 2 huku bao la nne likifungwa na Clement Mzize.

Ikiwa Afrika Kusini Yanga walicheza michezo mitatu, wameshinda miwili na kupoteza mmoja tena na timu ngumu kutoka Ujerumani FC Augsburg.

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Acha ujumbe