Pulisic Anukia United Januari

Christian Pulisic anaripotiwa kuachana na Chelsea na kujiunga na wapinzani wao wakuu Manchester United katika dirisha dogo la usajili la Januari.

 

Pulisic Anukia United Januari

Licha ya kuanza mechi tatu pekee za Ligi Kuu msimu huu, Pulisic ameichezea Marekani kwenye Kombe la Dunia, akipachika bao na kusaidia Taifa lake kufuzu katika hatua ya 16 bora ya michuano hii.

Pulisic mwenye umri wa miaka 24 alifunga bao pekee la ushindi dhidi ya Iran siku ya Jumanne, ambalo liliwafanya waungane na Uingereza katika kundi hilo B ambao wamefuzu.

Ingawa anachukuliwa kuwa mchezaji wa mechi moja moja Taifa lake litamenyana dhidi ya Uholanzi siku ya Jumamosi katika hatua ya 16 bora na inaonekana uchezaji wake tayari umechochea nia ya baadhi ya timu kutaka huduma yake.

Pulisic Anukia United Januari

Taarifa kutoka Italia zinasema kwamba, wababe wa Serie A Juventus wamewasiliana na London ya Magharibi kuhusu uhamisho wa Pulisic majira ya baridi na pia wanawasiliana na wakala wa mchezaji huyo.

Hata hivyo, ripoti hiyo hiyo inadai kuwa ni Manchester United ambao wako katika nafasi nzuri ya kusaini huku Ten Hag akisema yuko tayari kuimarisha safu yake ya ushambuliaji Old Trafford Januari baada ya mkataba wa Cristiano Ronaldo kuvunjwa mwezi uliopita.

United waliuliza kuhusu Pulisic msimu uliopita wa joto lakini hakuna mpango uliofikiwa, ingawa mchezaji huyo anafikiriwa kuwa anataka kusalia kwenye Ligi ya Uingereza.

Pulisic Anukia United Januari

Chelsea wangetaka makubaliano ya kudumu kuafikiwa iwapo wataruhusu namba 10 kuondoka, huku pauni milioni 35 ikitajwa kuwa bei inayotarajiwa na mchezaji huyo amebakiza miezi 18 tu kukamilisha mkataba wake wa sasa Stamford Bridge na haonekani kuwa mchezaji pendwa wa Graham Potter.

Pulisic, ambaye ana mabao 22 ya katika mechi 55 alizocheza Marekani, alitupia mabao 21 katika mechi 34 katika msimu wake wa kwanza kamili akiwa na Chelsea lakini ameshindwa kufikia viwango hivyo tangu wakati huo.

Pulisic Anukia United Januari


Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

BONYEZA HAPA KUCHEZA

 

 

Acha ujumbe