Klabu ya Simba itacheza mchezo wa kirafiki hii leo dhidi ya Malindi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Stadium majira ya saa 2 na robo usiku, ambapo mechi hiyo itakuwa ya kujiimarisha kujiandaa na mechi zijazo za Ligi pamoja na Klabu bingwa.
Simba alienda Zanzibar Jumamosi baada ya kualikwa na baadhi ya timu za hoko kisiwani Zanzibar kwaajili ya mechi hizo, huku ligi zikiwa zimesimama kwa muda kupisha klalenda ya FIFA ambayo inahusisha timu za Mataifa mbalimbali kucheza mechi za kuwania kufuzu na kirafiki.
Baada ya kucheza mechi ya leo Wekundu wa Msimbazi, watavaana Kipanga ambao ni wawakilishi katika michuano ya CAF, lakini pia kocha Mgunda akizidi kuwaangalia vijana wake wanavyojituma viwanjani huku akiwa na kibarua kizito kuchagua nani aanze na nani asubiri benchi.
Simba mpaka sasa kwenye ligi kuu wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 10, sawa na wapinzani wao Yanga huku tofauti yao ikiwa ni amagoli ya kufungwa na kufunga. Pia akiwa ametoa sare moja. Na katika uapnde wa michuano ya klabu bingwa ameshinda michezo yake yote miwili ya mwanzo. Hivyo anasubiri kumenyana na Primeiro De Agosto ya Angola katika hatua inayofuata ya michuano hiyo.