Mechi ya Watani wa Jadi ambayo Yanga na Simba SC wanaikumbuka sana ilikuwa ni mechi ambayo Yanga ikishinda au kupata sare inakuwa Bingwa wa ligi, Simba ikipoteza mechi inashuka daraja!

Hiyo ilikuwa mwaka 1988, Simba SC ilikuwa na alama 20 nafasi ya tatu kutoka mkiani wakiwa kwenye hatihati ya kushuka daraja. Yanga ilikuwa inakimbizana na Costal Union kuwania ubingwa.

simba

Ndipo timu hizi zikakutana kwenye mchezo wa Watani wa Jadi, kumbuka Yanga ikishinda inakuwa bingwa na Simba akipoteza anashuka daraja.

Wananchi walihitaji alama moja pekee kushinda ubingwa kwa sababu Coastal Union ilishapoteza mechi dhidi ya African Sports.

Simba SC ilitangulia kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Edward Chumila lakini wananchi wakasawazisha kupitia kwa Issa Athumani.

simba

Kipindi cha pili Simba ilipata bao la pili lililofungwa na John Makelele na mechi ikamalizika Mnyama ikishinda 2-1 na kubaki ligi daraja ka kwanza. Yanga ikapoteza ubingwa kwa tofauti ya magoli dhidi ya Coastal Union baada ya kulingana pointi.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa