Kimahesabu, ni takribani pointi 12 zinazowaniwa kuelekea mwishoni mwa msimu wa 2021/22 kwenye EPL, nani atatoboa?

Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa, ni ushindani sehemu zote. Mbio za ubingwa, nafasi ya 4 nayo ni lulu ya aina yake. Katikati ya msimamo napo kuna vitu ya aina yake kama ambavyo nafasi za mwisho zilivyo na safari za kupigana vikumbo.

Ni dhahiri, vita ya kutwaa ubingwa wa Ligi ipo kati ya Manchester City na Liverpool, ni tofauti ya pointi 1 tu inayomueweka City kwenye uongozi lakini, Liverpool anaongoza kwa idadi ya magoli akimzidi City kwa goli 1 pekee. Nani atavuna pointi nyingi kati ya 12 walizobakiza?

EPL, EPL Burudani Inanoga Mwishoni!, Meridianbet

Burudani ya kuitafuta top 4 ipo kwa Arsenal vs Spurs, kunatofauti ya pointi 2 tu kati yao. The Gunners wanaishikilia nafasi ya 4 kwa sasa wakiwa na pointi 63, pointi 3 pungufu ya Chelsea katika nafasi ya 3. Spurs nao sio wanyonge, wanapointi 61 wakiwa nafasi ya 5. Pengine kitakachoamua hatma yao ni mchezo wao dhidi ya Arsenal, huenda Chelsea akaingia kwenye mkumbo wa kuisaka nafasi ya 4 endapo ataendelea kupoteza pointi kuelekea mwishoni mwa msimu huu.

EPL, EPL Burudani Inanoga Mwishoni!, Meridianbet

Nafasi ya 6 na 7 ni mwendo wa kuombeana mabaya kati ya Manchester United, West Ham United na Wolverhampton Wanderers. Kunatofauti ya pointi 3 kati ya United na The Hammers kwenye nafasi ya 6 na 7. Nyuma yao yupo Wolves ambaye anapointi 49 akiwa na mchezo mmoja pungufu ya watungulizi wake. Ule msemo wa kila mtu ashinde mechi zake unaanza kuonekana kunako EPL.

EPL, EPL Burudani Inanoga Mwishoni!, Meridianbet

Norwich City washaijua hatima yao msimu huu, wanashuka daraja. Swali ni nani ataungana nao? Hapa kuna takribani timu 4 ambapo, 2 kati yao zitaungana na The Cannaries kuondoka kwenye EPL.  Everton, Burnley, Watford na Leeds zipo kwenye mchakato huu. Newcastle alikua huku lakini sasa hivi ameshajinasua na yupo mbali kwenye kifungo hiki, nani atajinusua? EPL inanoga!!


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa