Pengine sio miongoni mwa watu wanaopewa sifa na heshima wanazostahili lakini, makocha ni watu muhimu kwenye vilabu. Carlo Ancelotti ameweka historia barani Ulaya.

Ukimtizama kwa haraka haraka, humuoni kama mtu wa kazi lakini, Ancelotti ni kocha wa aina yake. Mbinu zake za kuviongoza vilabu ni upekee wa aina yake, anatofauti kubwa na makocha wengine wa kaliba yake.

Kwa sasa ulimwengu unawaongelea zaidi Pep Guardiola na Jurgen Klopp, pengine ni kutokana na wigo mpana wa kuipigia chapuo ligi ya Uingereza (EPL) lakini, kuna mbabe wao kwenye bara zima la Ulaya.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Carlo Ancelotti apewe heshima yake kwenye soka. Ni zaidi ya nguli kwenye vitabu vya historia, hakika Ulaya itamkumbuka kwa karne na karne.

Je wajua? Carlo Ancelotti ametwaa mataji yote 5 kwenye ligi 5 bora za soka barani Ulaya? Naam, kama hukua unafahamu sasa chukua hiyo.. Kombe la 35 la LaLiga kwa Real Madrid wikiendi hii, limekamilisha historia ya kocha huyu barani ulaya.

Ancelotti

Alibakiza taji la LaLiga tu akiwa tayari ameshatwaa taji la EPL (alipokua na Chelsea), Bundesliga (alipokuwa na Bayern Munich), Ligue 1 ( alipokua na PSG) na Serie A (alipokua na AC Milan). Hakika, kurejea kwake Santiago Bernabeu msimu huu ni neema kwake na klabu hiyo.

Madrid wametangazwa mabingwa wa ligi wakiwa wamebakiza michezo 4 kumaliza msimu huu. Miamba hii ya soka barani Ulaya wanatwaa ubingwa wakiwa na tofauti ya pointi 17 na Sevilla ambayo inashikilia nafasi ya 2.

Ancelotti, Ancelotti Kinara Barani Ulaya, Meridianbet

Pengine historia inaweza ikanoga zaidi, kituo kinachofata ni hapo hapo Bernabeu kupambana na Manchester City katika mchezo wa marudiano kunako nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa. Kama Madrid watafanikiwa kutinga fainali na pengine kutwaa ubingwa, Ancelotti ataweka historia nyingine ya kuwa kocha pekee aliyefanikiwa kutwaa taji hilo mara 4.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa