Simba SC Yaja na Its Not Over, Kazi Iendelee.

 

Kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa, Klabu ya Simba SC imetambulisha slogan ya ‘Its Not Over, Kazi Iendelee.’

 

Slogan hii imekuja baada ya Simba SC kupata na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Jwaneng wikiendi iliyopita nchini Botswana ambapo imedai pamoja na matokeo hayo lakini bado kazi haijaisha.

Kaimu Msemaji wa klabu ya Simba SC, Ally Shatry ‘Chico’ amesema Jwaneng ni timu nzuri na itakuja kwa nia moja ya kutaka kupindua matokeo hivyo tumejipanga kuhakikisha tunawakabili na kupata ushindi.

Chico amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika kwa asilimia 90 kikosi kiko kambini na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo.

“Kama kawaida yetu kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa tunakuwa na slogan yetu na safari hii ni IT Is not Over, Kazi Iendelee. Hii ina maana kuwa tumepata ushindi ugenini lakini kuna dakika 90 nyingine Jumapili ambazo tunahitaji kupata ushindi, kazi bado inaendelea,” amesema Chico.

Chico ameongeza kuwa wapinzani wao Jwaneng tayari wametua nchini jana kimya kimya tayari kwa mchezo huo muhimu.

Viingilio vya mchezo huo ni Sh 5,000 mzunguko lakini ukinunua tiketi uwanjani itakuwa Sh 7,000, VIP B na C Sh 20,000 VIP A Sh 40,000 na Platinum Sh 150,000.


KUSANYA MKWANJA NA BIG BAD WOLF

Mchezo wa Big Bad Wolf ni moja ya michezo pendwa katika kasino zetu za meridianbet. Ukiachana na tabasamu utakalolipata wakati wa kucheza pia unajiwekea nafasi ya kuwa mshindi wa mkwanja mrefu unaotoka kila baada ya mzunguko kukamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.