Gomes : Kanoute, Sakho, Nyoni, Banda Tuwape Muda.

Kocha Mkuu Wa Simba SC, Didier Gomes amesema wachezaji wake wapya Pape Sakho, Duncan Nyoni na Peter Banda wanahitaji muda zaidi kuingia moja kwa moja kwenye kikosi chake.

 

Pape Sakho Muuaji Mpya Simba SC.

Sakho, Nyoni na Banda waliosajiliwa msimu huu hawaingii moja kwa moja katika kikosi cha Simba. Gomes alisema wachezaji hao ni wazuri na ndio maana walisajiliwa, lakini kucheza wanahitaji muda.

“Kikosi changu kina wachezaji wengi wapya msimu huu. Wanahitaji muda wa kuzoeana na wenzao na kufanya vizuri, lakini hadi sasa wanazidi kuwa bora kadri siku zinavyokwenda,” alisema Gomes.

“Sadio Kanoute, Sakho na Nyoni wanakuja vizuri na naamini watakuja kuleta vitu vizuri siku za mbele. Najiamini sana kutakuwa na mambo mazuri siku za mbele, wachezaji wote wanabadilika kiuchezaji.”

 

Gomes - Kanoute Amerejea Kuwavaa Galaxy.

Gomes alisema kuondoka kwa Clatous Chama na Luis Miquissone kunamtaka atengeneze aina nyingine ya washambuliaji ili timu iendelee kufanya vizuri.

“Tumeanza kubadilika eneo la ushambuliaji. Kiukweli kuondoka kwa Luis na Chama unatakiwa utafute njia nyingine ya kwenye ushambuliaji. Tupo njia sahihi mpaka sasa,” alisema.

 

Banda : Bocco Amenipa Motisha ya Kupambana.

Sakho kwenye mechi za mashindano alianza na Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga na mechi ya Dodoma Jiji ya Ligi Kuu Bara tu katika mechi tatu ambazo Simba wamecheza, huku Banda aliingia dhidi ya Yanga (Ngao ya Jamii) na mechi ya Biashara na Dodoma Jiji. Naye Nyoni aliingia akitokea benchi katika Ngao ya Jamii, Biashara na Dodoma Jiji.


KUSANYA MKWANJA NA BIG BAD WOLF

Mchezo wa Big Bad Wolf ni moja ya michezo pendwa katika kasino zetu za meridianbet. Ukiachana na tabasamu utakalolipata wakati wa kucheza pia unajiwekea nafasi ya kuwa mshindi wa mkwanja mrefu unaotoka kila baada ya mzunguko kukamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.