Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele, yuko tayari kuhamia Newcastle United wakati mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa, 24, alijiunga na klabu hiyo ya Catalan kwa ada ya £117m mwaka 2017.

Newcastle imemfanyia usaili kocha wa zamani wa Roma Paulo Fonseca kupitia njia ya mtandao wa Zoom, mreno huyo mwenye umri wa miaka 48 anaonekana kuongoza katika makocha wanaowaniwa kumrithi Steve Bruce.

Tetesi zinasema, Chelsea wanamtaka mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21, kutoka Borussia Dortmund, anasema kocha wa timu hiyo Thomas Tuchel.

 

Barcelona

Tetesi zinasema, Manchester City wanamsaka mshambuliaji wa Fiorentina, Mserbia Dusan Vlahovic, 21.

Vilabu vya Manchester City na mahasimu wao Manchester United vinafikiria kuchuana na Barcelona katika mbio za kusaka saini ya mshambuliaji wa RB Leipzig na Hispania Dani Olmo.

Kiungo wa Leicester City Mbelgiji Youri Tielemans, 24, amekataa ofa ya kuongeza mkataba, na kuvifanya vilabu vya Manchester United, Chelsea, Liverpool, Real Madrid, Atletico Madrid na Bayern Munich kukaa mguu sawa.

Brighton wanamfuatilia mshambuliaji wa Clermont raia wa Guinea, Mohamed Bayo, 23, ambaye klabu yake hiyo ya Ufaransa inataka ada ya £10m, Bayo amekuwa akifananaishwa na mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku.

 

Bruno Fernandes Atimiza Ndoto Man United
Bruno Fernandes (Man United)

Kiungo mreno Bruno Fernandes, 27, alitishia kuondoka baada ya kusikia klabu yake ya Manchester United ilikua moja ya vilabu 12 vilivyosaini mpango wa kuanzishwa kwa ligi mpya ya Ulaya European Super League.

Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27, anakaribia kabisa kusaini mkataba mpya na vigogo wa Italia Juventus, anasema makamu wa rais wa klabu hiyo Pavel Nedved.

Tetesi zinasema, Sheffield United bado wanamuania kumsajili winga wa Barcelona, mhispania Alex Collado, 22 baada ya kushindikana kumsajili katika dirisha lililopita la majira ya joto.


KUSANYA MKWANJA NA BIG BAD WOLF

Mchezo wa Big Bad Wolf ni moja ya michezo pendwa katika kasino zetu za meridianbet. Ukiachana na tabasamu utakalolipata wakati wa kucheza pia unajiwekea nafasi ya kuwa mshindi wa mkwanja mrefu unaotoka kila baada ya mzunguko kukamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.