Simba SC Yaondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Klabu ya Simba SC imekubali kipigo cha mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy na kutolewa katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo itashiriki Kombe la Shirikisho.

Matokeo hayo yamewafanya kuwa sawa kwa jumla ya mabao 3-3 lakini Galaxy wanasonga mbele kwa faida ya bao la ugenini kutokana na ushindi wa 2-0 tuliopata kwenye mechi ya kwanza.

Mchezo wa hapo jana ulianza kwa kasi kwa Simba SC kuliandama lango la Jwaneng katika dakika 15 za kwanza na kutengeneza nafasi kadhaa ambazo hazikuzitumiwa vizuri.

Rally Bwalya aliiandikia Simba SC bao la kwanza dakika ya 40 baada ya kuwaacha walinzi na kuachia shuti kali ndani ya 18 lililomshinda mlinda mlango Ezekiel Morake.

Kipindi cha pili Jwaneng walirudi kwa kasi na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 46 kupitia kwa Rudath Wendell baada ya wenyeji kuchelewa kujipanga kabla ya kuandika bapo la pili dakika ya 59.

Dakika ya 85 Gape Mohutsiwa aliwafungia Galaxy bao la tatu kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Lesego Keredilwe.

Kocha  wa Simba SC, Hitimana Thiery aliwatoa Hassan Dilunga, Taddeo Lwanga, Bernard Morrison na Sadio Kanoute kuwaingiza Peter Banda, Erasto Nyoni, Duncan Nyoni na Meddie Kagere.


MCHONGO WA PESA NA CIRCUS FEVER

Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe