Tetesi zinasema, Beki wa kushoto Mbrazili Marcelo, 33 ameiambia Real Madrid kwamba ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huku huenda akatua katika klabu ya Fluminese ya nyumbani Brazil.
Klabu za Everton na West Ham ni miongoni mwa vilabu vinavyomuwania winga wa Inter Milan Ivan Perisic, 32. Hata hivyo vilabu vya ligi kuu ya Ujerumani-Bundesliga vimeonyesha pia nia za kumtaka Mcroatia huyo.
Tetesi zinasema, Newcastle United itapaswa kuweka mezani ofa ya kipekee na isiyo ya kawaida kumpata bosi wa Ajax, Erik ten Hag ili awe Kocha wao mpya.

Kiungo wa Angers Angelo Fulgini anavivutia vilabu vya ligi kuu England baada ya mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 25 kufunga goli dhidi ya Paris St-Germain mwishoni mwa juma lililopita.
Tetesi zinasema, Kocha wa West Ham, David Moyes ameonya kwamba klabu yoyote inapaswa kulipa kitita kinene cha zaidi ya £100m ili kumsajili kiungo wa England Declan Rice.
Tetesi zinasema, Chelsea imeulizia kuhusu upatikanaji wa winga Luis Diaz lakini klabu za Newcastle, Bayern Munich na Real Madrid pia zimewasiliana na wawakilishi wa winga huyo mwenye miaka 24.

Kiungo mfaransa Tanguy Ndombele, 24, anasema kikao cha mgogoro na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy kiliokoa maisha yake ya soka pale Tottenham Hotspurs.
Tetesi zinasema, mazungumzo kati ya Paul Pogba, 28 na Manchester United kuhusu mfaransa huyo kusaini mkataba mpya yamesimamishwa mpaka mwezi April na wakala wake Mino Raiola.
Mlinzi wa kati wa Chelsea Antonio Rudiger anatajwa kutaka kuondoka Stamford Bridge msimu ujao huku Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 28 akihusishwa na vilabu vya Juventus, Manchester City, Tottenham na Paris St-Germain.
Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.

Cheza hapa

