Steven Gerrard Anasubiri kwa Hamu Kuinoa Liver Endapo Arne Slot Akifutwa Kazi

Gwiji wa Liverpool FC, Steven Gerrard, anaripotiwa kusubiri simu akingoja mwaliko kutoka kwa klabu yake ya zamani ili achukue nafasi ya kocha wa dharura hadi mwisho wa msimu, kwa mujibu wa Indy Kaila.

Steven Gerrard Anasubiri kwa Hamu Kuinoa Liver Endapo Arne Slot Akifutwa Kazi

Utetezi wa taji la EPL wa Liverpool ulianza vizuri kwa ushindi mara 5 mfululizo, lakini baadaye wakaanza kupoteza mechi kadhaa huku mbinu yao ya kushambulia bila kujali ulinzi ikianza kuwaathiri.

Hadi sasa msimu huu, kikosi cha Arne Slot kimepoteza mechi tisa, na ingawa wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, wako kwenye ushindani mkali wa kufuzu UEFA Champions League, wakiwa kati ya timu imara kama Aston Villa na Chelsea FC.

Kumekuwa na tetesi za muda mrefu kuhusu presha kwa kocha huyo Mholanzi, huku udhaifu wa timu yake ukiendelea kuonekana, na kuruhusu Tottenham Hotspur kusawazisha dakika za mwisho Jumapili hakujasaidia hali hiyo.

Liverpool walikuwa mbele kwa 1-0 dhidi ya Spurs waliokuwa wanapambana kushuka daraja kuanzia dakika ya 18 hadi ya 90, ambapo Richarlison alifunga bao la kusawazisha na kuwanyima ushindi.

Steven Gerrard Anasubiri kwa Hamu Kuinoa Liver Endapo Arne Slot Akifutwa Kazi

Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.

Inaelezwa kuwa Slot bado yuko salama kwa sasa, lakini endapo Liverpool wataamua kufanya mabadiliko ili kuimarisha mwisho wa msimu, Gerrard yuko tayari kusubiri nafasi hiyo.

Chanzo cha ndani, Indy Kaila, kinasema Gerrard yuko karibu na simu hivi sasa akisubiri kwa hamu kubwa kupokea wito wa Liverpool ili achukue jukumu la kocha wa muda hadi mwisho wa msimu. Inasemekana pia yuko tayari “kuacha kila kitu” ili kuiokoa klabu yake ya zamani.

Hata hivyo, licha ya kuwa gwiji wa klabu, Gerrard haonekani kuwa chaguo lenye msisimko mkubwa kama ilivyotarajiwa hapo awali. Katika msimu wake wa mwisho nchini Saudi Arabia akiwa na Al-Ettifaq, timu yake ilimaliza nafasi ya sita. Aidha, katika uzoefu wake wa mwisho England akiwa na Aston Villa, alimaliza nafasi ya 14 na baadaye kufutwa kazi baada ya kushindwa kuonyesha maendeleo.

Steven Gerrard Anasubiri kwa Hamu Kuinoa Liver Endapo Arne Slot Akifutwa Kazi

Kutokana na matokeo hayo ya hivi karibuni, kuna maswali iwapo kurejea kwake Liverpool kutaleta tofauti katika timu inayopitia wakati mgumu.

Kwa upande mwingine, Slot amesisitiza kuwa anapata sapoti kubwa kutoka kwa klabu. Alieleza kuwa licha ya changamoto za msimu huu, bado anahisi kuungwa mkono na mashabiki, viongozi na watu wote ndani ya klabu.

Aliongeza kuwa Liverpool ni sehemu nzuri kufanya kazi kutokana na mazingira, watu na mashabiki wake, na hata katika kipindi kigumu kama hiki, bado ni heshima kuwa sehemu ya klabu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.