Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)  imeshinda hapo jana bao 1-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda the Cranes katika mchezo wa kirafiki wa klaenda ya FIFA ulipigwa katika uwanja wa Modern Benghazi, Libya.

Tanzania Yashinda Dhidi ya Uganda

Bao hilo pekee lilipigwa na Simon Msuva na ndilo lilidumu hadi dakika za mwisho, ambapo timu hiyo ikifanyiwa mabadiliko ya wachezaji kadhaa ambapo katika nafasi ya golikipa ilichukuliwa na golikipa namba mbili wa Simba Beno Kakolanya.

Hatahivyo imekuwa ni furaha kwa timu ya Tanzania kushinda mbele ya Uganda kwani mechi mbili za mwisho Taifa Stars ilipoteza kutoka kwa Uganda, na mchezo unaofuata atacheza na Libya mchezo wa kirafiki katika ratiba ya FIFA.

 

Tanzania Yashinda Dhidi ya Uganda

Baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Taifa Stars Honour Janza aliwazungumzia Uganda akisema ni timu nzuri, na ni hatari kwani wana uwezo wa kufosi pale panapotakiwa na ni wagumu pia kwani wako fiti.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa