LICHA ya kuwa kwenye kikosi cha TP Mazembe inayoshiriki ligi kuu ya Congo, aliyekuwa kiungo wa Yanga, Mukoko Tonombe amesema kuwa anatamani ligi kuu ya Tanzania.

Tonombe alikitumikia kikosi cha Yanga kwa misimu kadhaa kwa mafanikio makubwa ambapo pia alikuwa nahodha wa timu hiyo.

 

Tonombe: Nimemisi ligi ya Tanzania

Alizungumza hayo baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Azam FC uliopigwa jana ijumaa kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola, nchini Zambia ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

 

Tonombe: Nimemisi ligi ya Tanzania

Akizungumza kutoka nchini Zambia, Mukoko amesema kuwa “Nimefurahi sana kucheza na timu kutoka Tanzania.

“Nimeikumbuka sana ligi ya Tanzania na wachezaji wengi ambao niliwahi kucheza nao lakini pia vyakula nimevikumbuka sana.”

 

Tonombe: Nimemisi ligi ya Tanzania

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa