ALIYEKUWA nyota wa Yanga, Mukoko Tonombe ambaye kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya TP Mazembe amepewa zawadi ya jezi na Uongozi wa Azam FC.

Tonombe alikitumikia kikosi cha Yanga kwa mafanikio makubwa ambapo aliondoka ndani ya klabu hiyo na kutimkia TP Mazembe kwa makubaliano maalum.

Azam, Tonombe Apewa Zawadi na Azam, Meridianbet

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka zakazi’ ndiye aliyekabidhi jezi hiyo leo wakati Azam wakicheza mchezo huo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe.

Mchezo huo wa kirafiki umepigwa kwenye Uwanja wa Ndola nchini Zambia huku timu hizo zote zikicheza zikitarajia kushiriki michuano ya kimataifa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa