UONGOZI wa klabu ya Pan African umefunguka kuwa mipango yao ni kupata matokeo kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Mashujaa.

Timu hizo zinakutana zikiwa zinafanana kwa pointi kila mmoja akiwa nayo moja ambapo wanatarajia kucheza kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi hicho, Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema kuwa: “Kikosi tayari kimefanya mazoezi ya mwisho leo Ijumaa kwenye uwanja ambao tutacheza mechi kesho.

“Wachezaji wana morali na ari kubwa kuelekea kwenye mchezo huo na hiyo inatokana na matokeo ya mechi iliyopita dhidi ya Kitayosce.

“Imani ni kubwa ya kupata matokeo kwenye mchezo huo na tunawaomba mashabiki wetu waje kutushangilia kesho.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa