Klabu ya As Vita ya DR Congo imetangazwa mabingwa wa DR Congo kwa msimu wa 2020/21 baada ya kushinda kesi yao CAS ya kupinga kuvuliwa ubingwa. As Vita ilipokonywa pointi 9 baada ya kusemekana kumtumia mchezaji Zao Matutala ambaye alikuwa na utata kwenye usajili wake.
Baada ya kupokonywa pointi 9 klabu hiyo ilimaliza nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini DR Congo nyuma ya TP Mazembe na Maniema Unioni. Kumaliza nafasi ya 3 iliipa faida klabu ya Simba SC ya Tanzania kuanzia raundi ya kwanza ya klabu bingwa Afrika (CAF Champion League).
Kwa Nini?
Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) lilipanga timu 10 (mojawapo Simba) ambazo zilikuwa juu kwenye club ranking kuanzia raundi ya kwanza. Simba kwenye Club ranking ilikuwa ya 15 ila kwenye timu 54 ambazo zinashiriki CAF Champion League Simba ipo nafasi ya 10 ndio maana ilipata nafasi ya kuanzia raundi ya kwanza.
Timu 5 ambazo zilikuwa juu ya Simba kwenye Club ranking zilikuwa zinashiriki mashindano ya shirikisho (Caf Confederation Cup) kati ya hizo tano mojawapo ilikuwa As Vita Club ya DR Congo iwapo isingepokonywa pointi 9 na kumaliza nafasi ya kwanza kwenye ligi ingeshiriki ligi ya mabingwa.
Kwa sasa ushindi wa As Vita Club huko CAS hauwezi kuiathiri Simba kwani shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) haliwezi kubadili ratiba yao zaidi ya As Vita atapewa ubingwa wa DR Congo tu na itashiriki mashindano ya kombe la shirikisho (CAF Confederation Cup) kama alivyopangwa awali.
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.


