Messi : Nilishtukizwa Kuondoka Barcelona.

 

Hatimaye Staa wa soka, Lionel Messi ameyaongea ya moyoni jinsi alivyolazimika kuondoka Barcelona katika mazingira ya kulazimishwa na ambayo hakuyatarajia ambapo kwenye Interview na CNN.

 

Messi amesema “Nilikua nimerudi Hispania baada ya michuano ya Copa America mwezi July, nilichokua nakiwaza ni kwamba mkataba huo uliwekwa pembeni sababu saini yangu tu ndio ilikua inasubiriwa kumbe sivyo”

“Nilipowasili Barcelona niliambiwa hilo la kusaini mkataba mpya haliwezekani tena hivyo nitafute klabu nyingine kwasababu klabu haiwezi kuniongezea mkataba, hilo lilinipa wakati mgumu sana nikaanza kufikiria mengi ikiwemo kubadilisha mfumo wa familia yangu kuacha makazi na kwenda kuanza sifuri kwenye sehemu nyingine”

“Kujiunga na PSG sikukosea, kilichonisaidia mimi kutulia baada ya kujiunga na PSG ni sura ninazozifahamu hapo na kuzingatia kwamba kuna wachezaji wengi wanaoongea lugha ya Kihispania kama ‘Ney’ ‘Lea’ (Paredes), ‘Fideo’ (Di Maria)” aliongeza Messi.


SPACE SPIN NA MERIDIANBET.

Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe