Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Newcastle United inawataka wachezaji wanne wa Manchester United wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari huku mashambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 25, kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 24, Beki wa Ivory Coast Eric Bailly na mshambuliaji wa England Jesse Lingard, 28, wote wakiwa katika orodha yao.

Naibu makamu wa rais wa klabu ya Barcelona Rafael Yuste amepuuza taarifa ya klabu hiyo ya Uhispania kumsajili mshambuliaji hatari wa Borussia Dortmund raia wa Norway Erling Braut Haaland ,21 msimu ujao.

 

Erling Braut Haaland: Real Madrid Wafikia Makubaliano
Erling Braut Haaland

Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 29, amesema kwamba huenda kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar likawa lake la mwisho , kwa kuwa mshambuliaji huyo wa PSG hana uhakika iwapo akili yake ina uwezo wa kukabiliana na changamoto za kandanda.

Tetesi zinasema, Barcelona huenda ikamuuza winga wa Ufaransa Ousmane Dembele iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hatoongeza nkataba mpya.

Juventus itamtumia kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 30, kama chambo cha kumvutia kiungo wa kati wa Manchester United na nyota wa Ufaransa Paul Pogba, 28, kurudi mjini Turin.

Tottenham inahusishwa na jaribio la kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Marekani Weston McKennie, 23, na mchezaji wa Uswidi mwenye umri wa miaka 21 Dejan Kulusevski kutoka Juventus.

Tottenham inamnyatia mshambuliaji wa Uhispania mwenye umri wa miaka 28 Alvaro Morata kuchukua mahala pake Harry Kane, 28. Morata kwasasa yuko Juventus kwa mkopo kutoka Atletico Madrid.

 

Juventus Hawakurupuki Kumsahili Morata

Tetesi zinasema, Liverpool iko tayari kuwasilisha ombi lao la kumsajili winga wa Wolves na Uhispania Adama Traore, 25.

Chelsea inakamilisha taratibu za kuongeza mkataba mpya na beki wa kati wa Denmark, Andreas Christensen huku makubaliano hayo yakiendelea kukamilishwa kabla ya kutangazwa rasmi.

Tetesi zinasema, Kiungo wakati wa Itali Marco Verratti, 28, anasema kwamba analenga kuhudumu kipindi chote kilichosalia katika klabu ya Ufaransa ya PSG.


Piga Mkwanja na LA Rouge

Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

CHEZA HAPA

Acha ujumbe