Roger Federer awashukuru mashabiki na wachezaji wenzake kwa kumpa kadi ntekundu ya “kimaaajabu” mwishoni mwa kazi yake nzuri ya kitaalamu siku ya Ijumaa.

 

Federer Awashukuru Mashabiki na Wachezaji

Bingwa huyo mara 20 wa Grand Slam alishusha pazia la maisha yake katika mechi ya wachezaji wawili wawili pamoja na Rafael Nadal kwenye Kombe la Laver jijini London wakikabiliana na Wamarekani wawili Jack Soack na Frances Tiafoe.

Ingawa Federer na Nadal walipoteza kwa 4-6, 7-6, (7-2) 11-9, maestro huyo wa Uswiz alipokelewa kama shujaa kwenye uwanja wa 02 Arena, na mpinzani wa zamani Nadal aliungana nae kumwaga machozi baada ya mchezo.

Federer Awashukuru Mashabiki na Wachezaji

Mara tuu baada ya hapo, Federer alitania kwamba alikuwa na furaha kwa kuepuka kuumia na akaelezea kazi yake kama “safari kamili”. Na baadae alionyesha shukurani zake kwa kila mtu aliyehusika Jumamosi akiandika kwenye Twitter: “Ilikuwa jioni ya kimiujiza jana” “Asante tena kwa mashabiki na wachezaji wote ambao walikuwa hapa kushiriki wakati huu nami. Inamaanisha Ulimwengu”.

Wakati huo Federer amekataa kushiriki mechi za  maonyesho katika siku zijazo, akisema nia yake ya kuruhusu mashabiki zake kumuona akiwa uwanjani kwa mara ya mwisho ambapo alisema kuwa ujumbe wake ulikuwa ni kuwasilisha mapenzi yake kwa mchezo huo kwa mashabiki na anatumaini kwamba wataonana tena nje ya uwanja wa tenisi.

Federer Awashukuru Mashabiki na Wachezaji

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa