Ten Hag Ampongeza Sancho kwa Kiwango Kizuri Alichokionyesha

Kocha mkuu wa Manchester United Erik ten Hag amempongeza Jadon Sancho kwa kiwango bora alichokionyesha kwenye mchezo wao wa jana ambao walitokea nyuma kwa mabao mawili na kuswazisha yote na kumalizika kwa 2-2 dhidi ya Leeds United.

 

Ten Hag Ampongeza Sancho kwa Kiwango Kizuri Alichokionyesha

Sancho alicheza mechi yake ya kwanza tangu Oktoba 22 alipoingia akitokea benchi dhidi ya Nottingham Forest mapema mwezi huu, baada ya kukosa muda mrefu kutokana na kile Ten Hag alichoeleza kuwa “hali za utimamu na hisia”.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uingereza aliingia kama mchezaji wa akiba katika kipindi cha pili na United ikifungwa 2-0 hapo jana, huku bao la mapema la dakika ya 1 la Wilfried Gnonto likifuatiwa na bao la kujifunga kutoka kwa Raphael Varane.

Hata hivyo, Marcus Rashford aliweka kambani bao lake la 20 msimu huu kabla ya Sancho kuweka la pili na kuwanyima Leeds ushindi ambayo imetoka kumtimua kocha wao hivi karibuni.

Ten Hag Ampongeza Sancho kwa Kiwango Kizuri Alichokionyesha

Ten Hag anatumai onyesho la Sancho ni ishara ya mambo yajayo, akisema juu ya utangulizi wake: “Nilitaka mabadiliko tofauti. Wakati huo hatukuwa mchezoni. Kwa bahati ilifanikiwa kwa sababu tulifunga mabao mawili. Tuna furaha sana, na Sancho amerejea. Tunajua ni mchezaji mzuri na nafikiri anaweza kuwa na athari kubwa mara kwa mara, lakini anatakiwa kufanya kazi kwa bidii.”

Ingawa Ten Hag alifurahishwa na kuimarika kwa United katika muda wote wa mechi, mwanzo wao wa polepole ulimfanya apate ladha mbaya, ikizingatiwa kwamba Gnonto alifunga wavu sekunde 55 tu baada ya kuanza.

Ni mwanzo mbaya sana, haukubaliki, haswa kwenye derby lazima uwe tayari kupigana na kuwajibika. Hatukufanya hivyo. Lazima niisaidie timu na uimara wao wa kupigana. Tulitengeneza mabao mawili ya timu kubwa. Alisema kocha huyo Mholanzi.

Ten Hag Ampongeza Sancho kwa Kiwango Kizuri Alichokionyesha

Baada ya kushuhudia Leeds wakitoa onyesho la kuvutia hapo jana Ten Hag aliitaka timu yake kushinda mechi nyingi zaidi wakati ujao.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.