Zlatan Ibrahimovic ameahidi kubadilika kwa AC Milan anapokaribia kurejea uwanjani baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu huku timu yake ikiwa inapiti magumu kwenye Serie A hadi sasa.
Ibrahimovic hajaonekana msimu huu, baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na jeraha alilolipata la anterior cruciate muda mfupi baada ya Milan kumaliza kusubiri kwa miaka 11 kushinda taji la Serie A mwezi Mei.
Wakati Milan walianza kwa heshima akiwa hayupo, wameteremka hadi nafasi ya sita kwenye Serie A wakiwa pointi 18 nyuma ya vinara Napoli baada ya kucheza mechi tano za ligi bila ushindi.
Hata hivyo, Ibrahimovic anaamini kuwa Milan wameshinda nyakati ngumu zaidi tangu aliporejea kwa mara ya pili katika klabu hiyo mwaka 2020, na anatarajia kurejea katika hali yake nzuri.
Ibarahimovic amesema kuwa; “Nilipowasili miaka mitatu iliyopita, watu walizungumza kuhusu hali ambayo ilikuwa mbaya zaidi kuliko sasa. Kwa kweli, sio mbaya kama watu wengine wanasema. Katika mwaka mmoja au miwili, tulifanya mambo ya ajabu, na bado tunafanya mambo mazuri.”
Mchezaji huyo amesema kuwa si kana kwamba kuna mtu amefurahishwa na fomu yao, bali wao wanafanya kazi kubadilisha mambo ili waweze kurejea jinsi walivyokuwa kabla ya Kombe la Dunia. Msimu huu ni tofauti kidogo, lakini tofauti kidogo lakini sio kisingizio.
Ibrahimovic aliiongezea Milan nguvu kubwa kwa kurejea kwenye mazoezi ya timu wiki iliyopita, ingawa inabakia kuonekana ni kwa muda gani anaweza kurejea kwenye hatua ya kiushindani, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 41 yuko mbioni kuondoka.
“Mimi ni mmoja wa wachezaji wengi katika timu hii. Sijapatikana kwa muda mrefu na hii imekuwa ya kukatisha tamaa kwa sababu unapokuwa mchezaji, huwa unataka kusaidia ndani na nje ya uwanja,”