Cantona: Ronaldo Anapaswa Kuwaiga kina Giggs, Ibrahimovic

Gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United Eric Cantona amesema staa wa zamani wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo anapaswa kuwaiga nyota kama Ryan Giggs na Zlatan Ibrahimovic.

Gwiji Cantona anasema kua Ronaldo anapaswa kukubali kua kwasasa hana miaka 25 tena hivo anapaswa kuishi kutokana na umri wake unavyotaka, Huku akiwatolea mifano wacheza kama Ryan Giggs pamoja na mshambualiji wa klabu ya Ac Milan Zlatan Ibrahimovic.CantonaGwiji huyo akimuongelea Zlatan Ibrahimovic ambaye bado anacheza katika klabu ya Ac Milan akisema mchezaji huyo amekubali kuishi kutokana na umri wake, Kwani mshambuliaji huyo amekua hapati nafasi mara kwa mara kwenye timu hiyo ila amekubali kutokana na kuelewa umri wake umesogea tofauti na Ronaldo.

Ronaldo aliachana na klabu ya Manchester United na kudai klabu hiyo imemsaliti na kudai hampi heshima kocha timu hiyo Erik Ten Hag, Staa huyo ambaye alikua hapati nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha Man United na ndio sababu kubwa ya staa huyo kuamua kuachana na klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Al Nassr.CantonaGwiji Cantona alisema kua kuna magwiji wa aina mbili ambao wanaamini bado wana miaka 25 na ambao wanajua umri umesogea na watasaidia vijana wadogo kama Ibrahimovic, Maldini na Giggs, Lakini ameeleza Ronaldo anafikiri bado ana 25 ndio maana anataka kucheza kila wakati jambo ambalo gwiji huyo anaona sio sahihi.

Acha ujumbe