Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Yanga Heritier Makambo ameagwa rasmi na klabu ya Yanga ikiwa ni wazi mchezaji huyo anakwenda kutafuta timu nyingine ya kuitumikia.
Mshambuliaji huyo ambaye amewahi kuitumikia klabu ya Yanga kwa vipindi tofauti amemalizana na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara klabu ya Yanga, Makambo raia wa kimataifa wa Congo inaelezwa anatafuta ya kuitumikia ndani ya ligi kuu ya NBC.
Klabu ya Yanga mpaka sasa imefanikiwa kuachana na washambuliaji wake wawili wa kimataifa ambao ni Makambo na Yacouba Sogne. Washambuliaji hao wameachw ana klabu ya Yanga kutokana na kukosa nafasi ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu sasa.
Mshambuliaji huyo atakumbukwa zaidi ndani ya klabu ya Yanga katika msimu wa 2017/18 ambao alikua kwenye ubora mkubwa akifanikiwa kua mfungaji bora wa klabu hiyo kabla ya kutimkia katika klabu ya Horoya Fc ya nchini Guinnea.
Makambo anaondoka ndani ya kikosi cha Yanga kutokana na kushindwa kugombania namba na mshambuliaji namba moja wa klabu hiyo Fiston Mayele, Hivo kumfanya mshambuliaji huyo kutafuta timu nyingine ambayo ataweza kupata nafasi ya kucheza.

