Klabu ya soka ya Yanga inaelezwa ina mpango wa kuachana na mshambuliaji wake raia wa Congo Heritier Makambo ambaye amekua hapati nafasi klabuni hapo.
Klabu ya Yanga imepanga kuachana na mshambuliaji huyo kwasababu ya mshambuliaji mwingine klabuni hapo ambaye amepona majeraha Yacoube Sogne, Na Yanga wanaona mshambuliaji huyo kutoka Burkinafaso anaweza kua na msaada mkubwa kuliko Makambo.
Mshambuliaji Yacouba Sogne inaelezwa ni pendekezo la mwalimu Nabi ambae alishauri mchezaji huyo asiachwe licha ya majeraha yake kua ya muda mrefu, Na sasa ndio anaonekana kua atakua na mchango mkubwa kuliko raia wa kutoka Congo Heritier Makambo.
Klabu ya Yanga pia imepanga kuepukana na gharama za mshahara kwani Makambo ni miongoni mwa wachezaji ambao wanalipwa vizuri ndani ya kikosi cha Yanga, Lakini amekua mchezaji ambaye hatumiki sana ndani ya kikosi cha mabingwa hao watetezi wa NBC.

