STRAIKA wa Yanga, Heritier Makambo ametoa ahadi kuelekea msimu ujao kwamba ataanzia pale alipoishia kwa msimu uliopita.

Makambo ni miongoni mwa wachezaji ambao wamejiunga na kambi hiyo mapema kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao.

Akizungumzia mazoezi yao, Makambo amesema kuwa mazoezi wanayoyafanya kwa sasa ni magumu lakini yatawafanya kuwa fiti zaidi kwa msimu ujao.

“Mambo yanaenda vizuri na tunajua ni maandalizi ya msimu ujao tunajua ni mazoezi magumu ila mwanzo ni mgumu hivyo inabidi tufanye ili tuwe fiti msimu ujao

“Msimu uliopita najua mambo hayakuwa mazuri sana lakini nina imani nitafanya vizuri zaidi kwa msimu ujao, ule mwisho wa msimu ulivyokuwa ndio nataka nianze hivyo.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa