KOCHA Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amefurahishwa na viwango vya wachezaji wapya ndani ya kikosi hicho akiwemo pia, Stephane Aziz Ki.

Yanga ambayo imeweka kambi Avic Town inaendelea na maandalizi ya msimu ujao wa 2022/23.

Wachezaji wapya ndani ya kikosi cha Yanga ni pamoja na Benard Morrison, Joyce Lomalisa, Lazarious Kambole, Gael Bigirimana na Stephane Aziz Ki.

Akizungumzia kambi yao, kocha Nabi amesema kuwa mazoezi yanaendelea vizuri na amefurahishwa na viwango vya wachezaji wake kwenye mazoezi hayo.

“Nimefurahi kwa ambacho nimeona kwa siku hizi ambazo tumefanya mazoezi hata kama kuna wachezaji ambao wanakosekana kwenye kikosi.

“Lakini pia nimefurahi kutokana na wachezaji kuwa fiti kwani wamefuatilia ileprogramu niliyowatumia walipokuwa likizo na pia nimefurahi kuona wachezaji wapya ambao wamesajiliwa kwenye kikosi kuwa fiti.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa