KUELEKEA kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Somalia, Kocha Mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen amemuongeza kikosini straika wa Geita Gold, Daniel Lyanga.

Mchezo huo wa marudiano wa michuano ya CHAN unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo Stars wakiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza.

Akizungumzia maandalizi yao, Kim amesema kuwa “Maandalizi  yanaendelea vizuri baada ya kumaliza mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Somalia tuliendelea na mazoezi ya kujiweka fiti.

“David Luhende tayari amerejea na ameanza mazoezi lakini kwa upande wa Aishi Manula bado hajaanza mazoezi.

“Lyanga ameungana na wenzake kwenye kikosi baada ya kumuita sio tu kwa ajili ya kufunga bali hata kutoa assisti na tunatarajia wataonyesha kiwango kizuri.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa