Manchester United Dimbani Leo

Klabu ya Manchester United leo itajitupa uwanjani kuwakaribisha klabu ya Nottingham Forest katika mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza baada ya michuano ya kombe la dunia.

Klabu ya Man United ambayo inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama 26, Huku wakiwa wamecheza michezo 14 ya ligi kuu ya Uingereza mpaka sasa na leo watacheza mchezo wa 15.manchester unitedKlabu ya Manchester United leo inakwenda kucheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu baada ya mapumziko ya kombe la dunia, Huku ikiwa na kumbukumbu ya kushinda michezo yake miwili ya mashindano huku mchezo mmoja ukiwa wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Fulham United kabla ya michuano ya kombe la dunia.

Klabu hiyo mpaka sasa wachezaji wake karibia wote waliokua kwenye michuano ya kombe la dunia wamerejea kasoro wachezaji watatu ambao ni Harry Maguire, Raphael Varane, pamoja Lisandro Martinez ambaye ameshinda taji la kombe la dunia akiwa na timu ya taifa ya Argentina.manchester unitedManchester United kwasasa wako kwenye mapambano ya kutafuta nafasi nne za juu ambazo walizikosa msimu uliomalizika, Ikiwa ni malengo ya mwalimu mpya ndani ya timu hiyo Erik Ten Hag ambaye moja ya malengo yake ni kuirejesha timu hiyo kwenye timu nne za juu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.