Eric Cantona alijiweka mbele kuwa ‘Rais wa soka’ wa Manchester United, lakini akakataliwa na mkuu wa zamani wa Utd, Ed Woodward.

Gwiji huyo wa Old Trafford alikutana na aliyekuwa makamu mwenyekiti mtendaji Woodward kabla ya kuacha wadhifa wake mwishoni mwa 2021 na akajitolea kuwa kinara wa klabu yake ya zamani.

 

Eric Cantona na Ndoto za Kuwa Rais wa Manchester United

Cantona alipendekeza kwamba Woodward na wengine wajikite kwenye upande wa masoko wakati yeye akifanya maamuzi yote ya soka, lakini wazo lake lilikataliwa.

Mwaka jana, nilipendekeza kwa klabu kubadili njia yao,’ Cantona aliambia The Athletic.

“Ed Woodward ni hodari katika masoko lakini si hodari katika soka. United wawe na mwenyekiti halafu wawe na rais wa masoko halafu rais wa soka ndiye mwenye maamuzi yote ya soka, kwa hiyo nilipendekeza kwao kwamba niwe rais wa soka”

 

Eric Cantona na Ndoto za Kuwa Rais wa Manchester United

“Nilikutana naye [Woodward] mara chache. Lakini hawakukubali! Bado nafikiria mimi au mtu mwingine, wanapaswa kuwa na mtu wa mpira wa miguu, inapaswa kuwa mtu kutoka klabu, ambaye anajua soka na klabu, lakini hawakutaka niwe rais wa klabu! Hawakunitaka! Na mashabiki wanapaswa kujua kwamba nilienda na kusafiri hadi Manchester ili kuwapa fursa ya kufanikiwa katika miongo ijayo. Na hawakutaka!”

Cantona alidokeza kwamba United wameongeza mapato yao maradufu tangu Sir Alex Ferguson alipostaafu 2013 lakini viwango vimeshuka uwanjani.

 

Eric Cantona na Ndoto za Kuwa Rais wa Manchester United

Klabu hiyo imeshindwa kushinda taji la Ligi Kuu tangu 2013, na mafanikio yao pekee ni ushindi mmoja wa Ligi ya Europa, Kombe la FA na Kombe la EFL.

Msimu uliopita ulikuwa wa janga kubwa ambapo Ole Gunnar Solskjaer alitimuliwa mnamo Novemba kufuatia mlolongo mbaya wa matokeo kabla ya timu kuendelea kuyumba chini ya usimamizi wa muda wa Ralf Rangnick.

Kocha mpya Erik ten Hag amekuja kujaribu kuirejesha United katika ubora wao wa zamani, na aliungwa mkono kwa paundi milioni 215 kwa ajili ya kusajiliwa kwa wachezaji wapya msimu wa joto.

Mshambuliaji Mfaransa Cantona, (56), alifunga mabao 82 katika mechi 185 akiwa na United kati ya 1992 na kustaafu mwaka 1997, akishinda mataji manne ya Ligi kuu na mawili ya FA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa