Carlos Alcaraz Atinga Nusu Fainali French Open.

Bingwa mtetezi wa French Open, Carlos Alcaraz, alionesha ubora wa hali ya juu kwa kumshinda Tommy Paul, na kufuzu kuingia hatua ya nusu fainali katika mashindano ya Roland Garros.

Carlos Alcaraz Atinga Nusu Fainali French Open.

Carlos Alcaraz ambaye ni mchezaji namba mbili kwa ubora duniani, alihitaji dakika 53 pekee kupata uongozi wa seti mbili kwa sifuri (2-0), akipoteza mchezo mmoja tu katika kipindi hicho.

Mmarekani Paul alionyesha upinzani mkubwa zaidi katika seti ya tatu, ingawa Alcaraz, mwenye umri wa miaka 22, alionyesha ubora wake baada ya kumdhibiti mpinzani wake huyo na kupata uongozi wa 5-4 kabla ya kukamilisha ushindi wa 6-0, 6-1, 6-4.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Mhisipania huyo sasa atakutana na Lorenzo Musetti mwenye umri wa miaka 23 katika hatua ya nusu fainali siku ya Jumapili.

Carlos Alcaraz Atinga Nusu Fainali French Open.

Musetti, mchezaji namba nane kutoka Italia, alifuzu kuingia hatua ya nusu fainali kwa kumtupa nje Frances Tiafoe kwa seti 6-2, 4-6, 7-5, 6-2 mapema Jumanne, na anaingia hatua hii ya nusu fainali ya Grand Slam kwa mara ya pili katika historia ya uchezaji wake baada ya ile ya Wimbledon mwaka 2024.

Katika mchezo wa robo fainali kati ya Musetti na Tiafoe, Tiafoe, ambaye ni Mmarekani wa kwanza kufika robo fainali ya French Open baada ya miaka 22, alifanikiwa kushinda seti ya pili baada ya Musetti kutawala seti ya kwanza.

Hata hivyo, mchezaji huyo anayeshika nafasi ya 15 alishindwa kuhimili kasi ya Musetti baada ya kupoteza seti ya tatu yenye ushindani mkali, na hakuweza kuendana na mtindo wa Musetti uliokuwa wa kuvutia lakini wenye mashambulizi makali.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.