Tottenham Yamuweka Sokoni Bergwijn.

 

Klabu ya Tottenham imefikia uamuzi wa kumuuza winga wake Steven Bergwijn mwezi huu katika harakati za kutaka kuimarisha kikosi hicho kwa kununua wachezaji wapya katika majira haya ya baridi.

 

Bergwijn ameichezea Tottenham mechi 13 pekee hadi sasa msimu huu na amekuwa akitumika kidogo tangu Antonio Conte achukue nafasi hiyo.

Winga huyo kwa sasa anauguza jeraha lakini vyombo mbalimbali vya habari za michezo vimeripoti Tottenham wamefanya uamuzi wa kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 mwezi huu.

Hizo ni habari njema kwa klabu ya Ajax, ambayo imekuwa ikifwatilia huduma za mchezaji huyo na kuonyesha nia ya kumsajili Bergwijn mwezi huu, huku Mholanzi huyo pia akitaka kuhamia Amsterdam.

Ajax wanapaswa kumuuza David Neres kwanza, huku Shakhtar Donetsk ya Uturuki wakiripotiwa kumtaka Mbrazil huyo.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe