Tanguy Ndombele anatarajia kuondoka Tottenham Hotspurs mwezi huu, kwa mujibu wa The Athletic.
Kiungo huyu alizomewa na mashabiki Jumapili baada ya kubadilishwa kwenye mechi dhidi ya Morecambe ya Kombe la FA. Mechi ambayo Spurs ilishinda bao 3-1.
Wakati klabu ikitajwa kuwa hajapendezwa na matendo ya Ndombele hivi karibuni, vyanzo kadhaa vina ainisha kuwa kuachana kwa pande hizi mbili ndiyo linaweza kuwa suluhisho.
Taarifa zinasema kuwa Ndombele aliwaambia Spurs kuwa anataka kuondoka klabuni hapo msimu wa joto, na wangeweza kumuweka sokoni mwezi huu ikiwa wangeweza kumpata mnunuzi.

Changamoto inabaki wa Spurs ambao walimsajili nyota huyu kwa dau la kuvunja rekodi kutoka Lyon la £55 Julai 2019, na mshahara wake ukiwa ni £200,000 kwa wiki. Mkataba wake unadumu hadi mwaka 2025.
Barcelona wameripotiwa kuwa wanavutiwa na huduma ya nyota huyu, lakini hawajawekeza kwenye lengo la kumsajili staa huyu msimu huu. Lakini ni matumaini ya staa huyu kuwa uhamisho wake utakamilika na vinginevyo ataendelea kupiga mzigo chini ya Antonio Conte.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

CHEZA HAPA

