United Wanaungana na Chelsea Kumuwania Leao

Klabu ya Manchester United wameungana na Chelsea katika mbio za kumnasa mshambuliaji wa AC Milan Rafael Leao mwenye umri wa miaka 23.

United Wanaungana na Chelsea Kumuwania Leao

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ureno, amebakiza miezi 18 katika mkataba wake wa sasa San Siro na amekataa ofa ya mkataba mpya wa miaka mitano ya kuendelea kusalia klabuni hapo.

Kulingana na The Daily Star United wako macho kufuatilia hali ya mchezaji huyo na sasa wako tayari kushindania kupata saini ya Leao na wapinzani wa Ligi kuu ya Uingereza na mashabiki wa muda mrefu Chelsea.

United Wanaungana na Chelsea Kumuwania Leao

Manchester United  wamekuwa na maskauti wakimtazama nyota huyo wa Serie A katika miezi ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na wakati wa mechi ya mfululizo ya Milan katika Ligi ya Mabingwa ambayo walipoteza kwa jumla ya mabao 5-0 michezo yote miwili.

Mzaliwa huyo wa Almada ni mmoja wa vipaji bora katika ligi kuu ya Italia, akiwa amefunga mabao manne na kutoa asisti tano katika mechi tisa za ligi kufikia sasa muhula huu. Pia alitajwa kuwa Mchezaji Bora wa Serie A msimu wa 2021-22, baada ya kufunga mabao 11 na kuisaidia Rossoneri kutwaa ubingwa wa Scudetto.

Huku Leao mwenye mechi 11 akitarajiwa kuichezea Ureno kama nyota kwenye Kombe la Dunia, ubora wake alionao unaweza kuwafanya wawaniaji wengi kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumsajili mchezaji huo nchini Qatar.

United Wanaungana na Chelsea Kumuwania Leao

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.