Beki wa kati wa Manchester United, Raphael Varane aliondoka uwanjani hapo jana huku akilia baada ya kuumia katikati ya mchezo wakati mechi ikiendelea kwenye mchezo wa Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Chelsea.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ufaransa alilazimika kutoka nje ya uwanja baada ya kuanguka vibaya huko Stamford Bridge huku ikiwa imesalia mwezi mmoja tuu kabla ya Kombe la Dunia nchini Qatar.
Varane alitoka nje huku akiwa amefunika uso wake akisindikizwa na wachezaji wenzake huku Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Ufaransa wakiwa na majeruhi kadhaa kabla ya kutetea taji lao walilolipata, wakati huo huo kiungo wa Chelsea, N’Golo Kante akikosa mchuano huo kutokana na jeraha la misuli ya paja.
Pia Kiungo wa Juventus, Paul Pogba bado hajarejea kutoka katika tatizo ambalo limemlazimu kusubiri kwa siku kadhaa baada ya siku si nyingi kocha Allegri kusema kuwa anaendelea vizuri.
Ufaransa wataanza kampeni zao za Kombe la Dunia dhidi ya Australia mnamo Novemba 22, kabla ya kumenyana na Denmark na Tunisia katika Kundi D.