Klabu ya Yanga SC leo wameingia kambini Avic Town Kigamboni kwaajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi kuu ya NPL dhidi ya Mbeya Kwanza utakao pigwa Sokoine, Jijini Mbeya, Novemba 30.
Yanga wataanza safari ya kuelekea Mbeya mnamo Jumapili kwa usafiri wa ndege kwaajili ya mchezo huo dhidi ya timu hiyo iliyopanda ligi kuu msimu huu.
Ofisa habari wa Yanga SC, Hassan Bumbuli amesema wachezaji wote wataingia kambini kuanzia leo mchana na watakua hapo mpaka siku ya kuelekea Mbeya kwaajili ya pambano hilo.
Wachezaji wa Yanga SC walipewa mapumziko mafupi baada ya kurejea kutoka Mtwara katika mchezo wa Ligi ya NPL uliotamatika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Namungo.
Kiungo wa Uganda, Khalid Aucho anatarajiwa kurejea katika kikosi hicho na atakuwepo katika mchezo unaofwata mara baada ya kupona jeraha lilomuweka nje kwa siku kadhaa.
Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.