Beki wa Barcelona Ronald Araujo ameripotiwa kuingia kwenye windo la Chelsea.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alijiunga na Barcelona kutoka klabu ya Boston River ya Uruguay mwaka 2018. Amecheza mechi 52 akiwa na Barcelona mashindano yote.
Araujo amekuwa mchezaji muhimu wa klabu yake kwenye msimu huu wa La Liga, akiwa amecheza mechi 13, klabnu yake inatajwa kuwa wanataka kumpatia mkataba mpya wa muda mrefu.
Hata hivyo, majadiliano juu ya mkataba mpya hayaonekani kuwa yamefikia hatua nzuri mpaka sasa, na mkataba wa sasa wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay Camp Nou unatarajiwa kumalizika Juni 2023.
Kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo, vilabu vingi vinaendelea kufuatilia kwa ukaribu hali hiyo, huku wakala wa beki huyo akipokea ofa nzuri kwa ajili ya mteja wake.
Ripoti hiyo inadai kuwa Chelsea inaonesha nia ya kutaka kumsajili Araujo, huku The Blues wakiamini kuwa ana sifa za kuwa imara katika soka la Uingereza.
Kikosi cha Thomas Tuchel kinaweza kuingia sokoni kumsaka angalau beki mmoja wa kati msimu ujao wa joto kutokana na kutokuwa na uhakika wa hatima ya Antonio Rudiger, Cesar Azpilicueta na Andreas Christensen.
Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.